user_mobilelogo

Party Emblem

Party Flag

 

Youth League

Contact us


Communist Party Marxist - Kenya (CPM-K)
This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O Box 101011-00101 Nairobi, Kenya.
 

Let's Get Social

          

 

Related Social Links

 Revolutionary Youth League (RYL)
   
 Revolutionary Student Commission
    
 Revolutionary Women League
 Pio Gama Pinto Institute 

Support CPM-K 

membership

Publications

 

 

 

 Grab a Copy

 

CPM-K Memberships

 

 

 

 

 

 

 

 

 

“Utekelezaji wa sera za kibepari nchini umetuumiza sisi wananchi tuliyo wengi. Ubinafsishaji wa ardhi, migodi, mbuga za wanyamapori na maliasili zingine umetupora sisi tuliyo wengi haki za umilikaji na matumizi ya ardhi zetu za jadi tulizozirithi kutoka kwa mabibi na mababu zetu. Badala yake serikali inashirikiana na wawekezaji (mabepari) wa nchini na wa kigeni kutunyonya, kutunyanyasa, kutuvunjia heshima, kuvuraga utamaduni wetu na haki zetu za binadamu kiholela. Mfumo wa ubepari na ubinafsishaji unaoendelea hauwezi kutukomboa kutoka kwa ufukara na kutuletea maendeleo endelevu kwani unapanua pengo kati ya matajiri na masikini. Lazima tujizatiti na kuungana kupambania kurudi kwa Azimio la Arusha!”.

Hayo na mengine yalisemwa na kuazimiwa na jamii za wakulima, wachungaji, mashirika ya umma na Watanzania makabwela ambao walishiriki katika Kongamano la Saba la tamasha ya wasomi ya kumuenzi baba wa taifa la Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Kongamano hilo lililofanyika kutoka tarehe 13 hadi 15 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Nkuruma katika Chuo Kikuu cha Dar - es - saalamu liliandaliwa na Kigoda cha Nyerere chuoni hicho chini ya uwenyekiti wa Profesa Peminah Mlama. Pamoja na watu kutoka mashinani, Kongamano hilo lilishirikisha wasomi na wanafunzi wa chuo kikuu na wa shule za upili ambao walilalamika jinsi wawoto wa makabwela wanavyozidi kunyimwa fursa ya kupata elimu bora kutokana na ubinafsishwaji wa taasisi za elimu nchini Tanzania. Wanafunzi wa chuo kikuu walilalamika kuhusu ukame wa demokrasi ya kitaaluma katika vyuo vikuu iliyoandamana na ubinafsishwaji wa elimu katika nchi hiyo. Kongamano hilo lilisisimuliwa na wanafunzi wa shule za upili waliyolalamika kwa ufasaha kuwa elimu sasa inawafundisha watoto maadili ya ubinafsi, ulafi na kutojali binadamu wengine badala ya yale ya kiutu na kizalendo yaliyokuwa yakifundishwa na mwasisi wa taifa lao, Nyerere.

Wawakilishi wa jumuia za wakulima na wachungaji kutoka Loliondo, Kilosa, Mbeya, Geita walieleza kwa uchungu kuhusu masaibu wanayolazimika kuishi nayo kutokana na kunyanyaswa na kuporwa haki juu ya ardhi na maliasili zao na wawekezaji wa Kitanzania na kigeni ambao sasa wanapendelewa na serikali dhidi ya jumuia. Kongamano lilisikitishwa na maelezo kuhusu uvunjwaji wa haki za binadamu za wakulima na wachungaji wanaoishi katika maeneo ya migodi ya Geita, Shinyanga na Mwanza. Kilio hichihicho kililiwa na wakulima makabwela wa mpunga kutoka Mbeya waliyonyang’anywa ardhi zao na wajasiriamali na serikali. Pia jumuia za wakulima na wachungaji za Kilosa katika Mkoa wa Morogoro zilisimulia jinsi dhuluma na migogoro ilivyozidi sehemu zao kutokana na uvamizi na unyakuzi wa ardhi unaoendelea kutokana na ubinafsishaji.

Aidha, wanaharakati wa kupigania haki za kijamii kutoka Kampala na Moroto Uganda walishiriki na vilevile mashirika ya umma ya Kenya mkiwemo shirika la haki za kijinsia, shirika la kupigania haki ya maji na shirika la kupigania haki ya ardhi ya umma huko Garissa. Nikiwa mwenyekiti wa chama cha Social Democratic Party of Kenya (SDP) niliongoza ujumbe wa wanachama wanne kushiriki kongamano hilo maarufu.

Mada kuu ya kongamano hilo ilikuwa ubinafsishaji na haki za kijamii. Shabaha ya mada hii ilikuwa ni kutathmini athari za kiuchumi, kisiasa, kijamii na kitamaduni za marekebisho ya kiuchumi yaliyotoa Tanzania kutoka barabara ya Azimio la Arusha (ujamaa) na kuitia katika barabara ya ubeparimamboleo. Baada ya Nyerere kung’atuka kutoka kwa urais wa Jamhuri ya Tanzania na pia uwenyekiti wa chama tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM), rais Ali Hassan Mwinyi aliyechukua nafasi yake alianza marekebisho ya kiuchumi ya kibepari katika nchi hiyo. Rais Benjamini Mkapa alimrithi Mwinyi na kuendelea kuzingatia sera za Rais Mwinyi za ruksa ya kuuvunja mfumo wa ujamaa na kujitegemea na kuelekeza Tanzania katika mfumo wa ubepari. Hivi leo Tanzania ikiongozwa na Rais wa nne Jakayo Mrisho Kiketwe inaendelea kutekeleza sera za ubepari na ukolonimamboleo kwa fujo.

Huku ikiwa katika mfumo wa ubepari, uchumi wa Tanzania umekua kwa kasi sana (kwa zaidi ya asilimia saba). Barabara nyingi za lami zimejengwa mijini na mikoani. Katika kila miji ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Dar - es - saalamu, Dodoma, Tanga, Mbeya, Arusha, Mwanza na Moshi majumba makubwa ya ghorofa yanaota kila kuchako. Aidha, mitaa ya kifahari wanakokaa matajiri yenye majumba makubwa na ya kupendeza ajabu nayo pia ni dhihirisho la kunoga kwa uchumi wa ubepari. Vilevile, masupamaketi ya kukidhia haja za tabaka la mabwanyenye na magari ya kifahari yamejaa kila sehemu mijini. Ardhi, migodi na mashirika ya umma yamezidi kubinafsishwa na kuuziwa (kupewa) mabepari wa Tanzania na nchi za kigeni. Wawekezaji kutoka kila pahali ulimwenguni wanakimbilia Tanzania kuwekeza na kununua mali ya umma ya viwanda, biashara, ardhi, madini, wanyamapori na maliasili zingine. Hata huduma za elimu, nyumba, maji, afya na umeme zimebinafsishwa.

Je, utekelezaji wa sera za ubepari umeathiri vipi tabaka la makabwela wa Tanzania? Washiriki wa kongamano la Nyerere walisema na kukubaliana kuwa ubinafsishaji wa uchumi kwa ujumla ni kinyume cha haki kwani unachukua mali inayomilikiwa na serikali kwa ajili ya wengi (umma) na kuwapa watu binafsi kwa kisingizio kimoja ama kingine. Marekebisho ya ubepari yamezidisha pengo kati ya matajiri na maskini, kupanda mbegu za uhasama wa kikabila  na kukiuka maadili ya kiutu yaliyozingatiwa na azimio la Arusha. Rushwa imekuwa dondandugu huku unyonyaji wa mtu kwa mtu ukiwa utamaduni wa kisasa. Wakati tabaka la wachache wanaotawala wakijilimbikizia utajiri mkubwa ajabu tabaka la Watanzania wengi linazidi kudidimia katika lindi la ufukara, shida na umkosefu wa kila hali. Washiriki kutoka Kenya, Malawi, Afrika Kusini na Uganda pia walisisitiza kwamba ubinafsishaji wa uchumi katika nchi zao pia umeleta manufaa kwa tabaka la wachache tu huku tabaka la wengi likizidi kusukumwa pembeni. Mwishowe kongamano liliamua kuwa ubepari umefeli Tanzania na pia Afrika Mashariki. Watanzania wengi hawana budi kupigania kurudi kwa Azimio la Arusha la siasa ya ujamaa na kujitegemea.

 

Mwandawiro Mghanga, Mwenyekiti wa Social Democratic Party of Kenya (SDP), Aprili 22, 2015

BONIFACE MWANGI, GUANTANAMO BAY, AND THE HYPOCRISY OF US SANCTIONS: STATEMENT TO...
23 May 2026 11:52

  The Communist Party Marxist Kenya notes the recent sanctions imposed by the United States government against a Tanzanian police official over the torture involving Kenyan activist Boniface Mwangi and Ugandan activist Agather Atuhaire.   As revolutionaries and defenders of democratic rights, we firmly condemn torture, arbitrary detention, repression, disappearances, and attacks against activists, workers, peasants, journalists, opposition forces, and progressive voices anywhere in Africa. The suffering of the people can never be normalised. State violence against the masses remains react [ ... ]

Read more
Fascism in the African Neocolonies Imperialist Crisis, and the Struggle for Nat...
22 May 2026 05:30

  Booker Omole, General Secretary, Communist Party Marxist Kenya
repared for the International Theoretical Conference on Fascism and Imperialism in the 21st Century in the Neocolonies
Kathmandu, Nepal
22 to 23 May 2026 Imperialism in Crisis and the Return of Fascism   The Communist Party Marxist Kenya extends militant proletarian greetings to all revolutionary organisations, communist parties, anti-imperialist formations, workers movements, youth organisations, and progressive intellectuals gathered at this important international theoretical conference in Kathmandu, Nepal.   This confe [ ... ]

Read more
STATEMENT OF THE CENTRAL COMMITTEE OF THE COMMUNIST PARTY MARXIST KENYA (CPMK) O...
19 May 2026 10:30

  The Central Committee of the Communist Party Marxist Kenya extends its highest revolutionary salute to the workers, students, boda boda riders, matatu workers, peasants, unemployed youth, and oppressed masses currently engaged in the ongoing General Strike and nationwide resistance against the unbearable conditions imposed upon the people by imperialism and its local comprador agents.   Today Kenya stands at a historic turning point.   The masses can no longer live in the old way. The ruling classes can no longer govern in the old way.   The sharp increase in fuel prices, transpo [ ... ]

Read more
THE DRIVE INTO WORLD WAR 3 AND THE WORLD ANTI IMPERIALIST FRONT
11 May 2026 07:14

  ate:  10b>th May 2026 Occasion: International Colloquium by World Anti-Imperialist Platform, Nairobi    Author: Booker Omole Position: General Secretary, Communist Party Marxist Kenya   E DRIVE INTO WORLD WAR 3 AND THE HISTORICAL EPOCH   Comrades, we are not living in ordinary times. We are living in a time of rupture, a time of transition, a time when the old order is decaying but refuses to die, and the new order is struggling to be born. The drive into a Third World War is not an accident. It is not a misunderstanding. It is not the result of individual leaders acting irr [ ... ]

Read more